Demmy Harmony Foundation Yafanya Usafi wa Mazingira Fukwe ya Magha Mbezi Beach B
Dar es Salaam — Katika kuunga mkono jitihada za utunzaji wa mazingira nchini, Timu ya Demmy Harmony Foundation imeshiriki katika zoezi kubwa la usafi wa mazingira katika fukwe ya Magha Mbezi Beach B, Dar es Salaam. Lengo kuu la zoezi hili lilikuwa ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ya bahari, kuondoa taka zote […]
Wanafunzi wa Themi Secondary School Wanufaika na Elimu ya Afya ya Hedhi Kutoka Demmy Harmony Foundation
Demmy Harmony Foundation (DHF) imefika katika Shule ya Sekondari Themi iliyopo Kata ya Themi, mkoani Arusha na kutoa elimu kuhusu afya ya hedhi pamoja na kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule hiyo wapatao 152. Bonyeza hapa kwa picha zaidi –> https://www.facebook.com/share/p/1GXgcRB5eC/
DHF Yaendesha Mafunzo ya Hedhi Salama na Kugawa Pads Kinondoni
Taasisi ya Demmy Harmony Foundation (DHF) Februari 27, 2026 imeendesha zoezi la utoaji wa elimu kuhusu hedhi salama kwa wanafunzi wa kike katika Shule ya Msingi Erastus – Bunju B, iliyopo Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Mbali na elimu hiyo, pia imegawa taulo za kike (pads) kwa wanafunzi ili kuwasaidia kujisitiri na kuendelea […]
DHF Yatoa Elimu ya Hedhi Salama na Kugawa Taulo za Kike Singida
Demmy Harmony Foundation (DHF) imeendesha zoezi la utoaji wa elimu kuhusu hedhi salama pamoja na ugawaji wa taulo za kike (pads) kwa wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Katala iliyopo Old- Kiomboi Wilaya ya Iramba mkoani Singida.