Dar es Salaam — Katika kuunga mkono jitihada za utunzaji wa mazingira nchini, Timu ya Demmy Harmony Foundation imeshiriki katika zoezi kubwa la usafi wa mazingira katika fukwe ya Magha Mbezi Beach B, Dar es Salaam.
Lengo kuu la zoezi hili lilikuwa ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ya bahari, kuondoa taka zote zinazochafua fukwe, pamoja na kuonesha mshikamano thabiti wa taasisi yetu katika kulinda ekolojia ya bahari.
Katika zoezi hilo, taka mbalimbali zilikusanywa na kuondolewa kwa usalama. Sambamba na usafi huo, timu ilitoa elimu ya vitendo kuhusu utunzaji wa mazingira kwa wananchi na wafanyabiashara waliokuwepo maeneo hayo, ili kujenga utamaduni endelevu wa usafi.
Kupitia hatua hizi, Demmy Harmony Foundation inaendelea kutimiza ahadi yake kwa jamii.
Demmy Harmony Foundation: Tabasamu na Jamii kwa mustakabali wa kesho!

Kwa habari zaidi: https://www.facebook.com/share/p/1Cjd9yK4Jd/