Call us for enquiry

+255 787 531 938

Mail us for enquiry

info@demmyfoundation.org

Maono ya Mwanzilishi wa Demmy Harmony Foundation

Habari,

Ninaitwa Demitria Gibure, wengi hupenda kuniita Demmy. Ni mama wa mabinti watatu, ni mwalimu, kwa sasa ninajihusisha na masuala ya afya ya jamii (CHW), naishi Ughaibuni (🤣🤦🏾‍♀️kwa watu) ila ni Mkwaya kyenekyene wa pale Mmhare Mwitongo, Nyumbani ni Mkinyerero jama.

Nilipata msukumo wa kuwashika mikono walimu wenzangu kwa kuanzia Wastaafu na wanaojitolea huko nyumbani kupitia Demmy Harmony Foundation ambapo tunarejesha Tabasamu kwa walimu hawa kwa namna mbalimbali kwa kugusa uhitaji wao ambao umo ndani ya uwezo wetu. Si kwamba walimu hawa ni wahitaji/tegemezi/wanyonge La-hasha, ni vile tu tunaitambua thamani na mchango wao mkubwa katika jamii yetu na kwa kuwatembelea na kuzungumza nao tunatambua ni maeneo gani haswa yanahitaji kuguswa ili kutunza tabasamu nyusoni mwao.

Tukumbuke walimu wetu walistaafu, wakakutana na wimbi la waroho wa pesa, wakawalaghai wawekeze pesa zao katika NGO zao eti ili zizae, ambapo wengine hadi sasa wamelizwa mno. Ila pia tukumbuke tunaishi kwenye familia zetu ambazo hadi mwalimu anastaafu bado kuna kizazi chake kinakuwa kinamtegemea haswa kwenye eneo lile ambalo akifikia ukomo wa utumishi anapoteza sifa za kupokea huduma fulani, mfano Bima za afya kwa wategemezi, ambayo wale wategemezi ambao wapo chini ya miaka 18 bado wanaihitaji haswa, hapo ndipo tunapoingia na kutafuta namna ya kumshika mkono mwalimu huyu.

Ila pia mwalimu huyu alitutoa katika wimbi la ujinga na kutupa mwanga wa kusoma, kuhesabu na kuandika jamani kwa nini tusirudi kwake😃

Mwalimu anayejitolea, anapata Posho kidogo ambayo haikidhi mahitaji yake ya kila siku, mwalimu huyu ni msaada mkubwa kwenye shule zetu na kwa kuunga mkono jitihada za serikali tumeona ni vema pia mwalimu huyu abaki na tabasamu.

Je, upo tayari kuungana nasi katika safari hii ya kurejesha tabasamu mwalimu kwa kumfanyia surprise mwalimu wako aliyestaafu/anayejitolea/aliyepo kazini? Kwa sasa tupo maeneo yafuatayo ambapo utaungana na mwakilishi wetu kuweka utaratibu mzuri wa kumfikia mwalimu huyo

  • Dar-es-Salaam – Bunju
  • Singida – Mjini
  • Iramba – Old Kiomboi
  • Tanga mjini – Kange
  • Handeni – Mdoe
  • Rufiji – Mbwara
  • Lindi – Matimba
  • Mtwara Mjini
  • Pwani – Kibaha
  • Mwanza – Ilemela
  • Musoma Vijijini – Nyakatende
  • Musoma Mjini – Kitaji
  • Dodoma – mjini
  • Njombe vijijini – Mtwango
  • Mji Njombe – Matola

Karibu inbox kwa utaratibu zaidi au wasiliana na Mkurugenzi Michael Nakuchima +255 787 531 938 au

Meneja Mawasiliano Dorice Merengo +255 746 321 382

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More Articles & Posts